You are currently viewing  RUWAZA YA BAADA YA 2030 YALENGA ZAIDI WANANCHI ASEMA RAIS

 RUWAZA YA BAADA YA 2030 YALENGA ZAIDI WANANCHI ASEMA RAIS

Rais William Ruto amesema mazungumzo ya kitaifa kuhusu mustakabali wa kenya baada ya Vision 2030 si mradi wa serikali, bali ni jukumu la kila mkenya.
‎Rais Ruto amesema mpango huo unapaswa kuundwa kwa ushiriki wa wananchi wenyewe, huku akisisitiza umuhimu wa maoni ya vijana, wafanyabiashara, wakulima, wataalamu, viongozi wa dini na makundi mengine ya jamii.

Akizungumza wakati wa mazungumzo ya kitaifa kuhusu beyond vision 2030, rais ruto amesema kenya ina fursa ya kuunda dira ya muda mrefu itakayolenga kuleta maendeleo endelevu na kuunganisha wananchi chini ya malengo ya pamoja.  

‎Amesisitiza kuwa dira hiyo haipaswi kubuniwa na wanasiasa au maafisa wa serikali pekee, bali inapaswa kuwa mpango unaomilikiwa na wananchi wote.