Kiongozi wa chama cha Roots Party, Prof George Lunchiri Wajackoya, amesisitiza kuwa ndiye mrithi wa Hayati Raila Odinga katika kumtimua Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Wajackoya anasema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, ulimpa msingi imara wa kumpa Rais Ruto ushindani mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Amezungumza katika eneo la Mlokhoni, kule Funyula katika Kaunti ya Busia, ambapo ameitaja kaunti hiyo ya mpakani kuwa ngome yake imara kwenye azma ya kuingia ikulu mwaka ujao.

