Seneta wa Nandi Samson Cherargei amesema wanaunga mkono kwa dhati azma ya Rais William Samoei Ruto ya kutafuta muhula wa pili wa uongozi
Cherargei amesema hana wasiwasi kuhusu maandalizi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, akiwahakikishia wakazi wa Nandi kuwa wana imani kubwa kwamba watafanikiwa kumsaidia Rais Ruto kupata muhula wa pili. Kauli hiyo inaendeleza msimamo wake wa kumuunga mkono Rais Ruto kuelekea uchaguzi ujao.
Seneta huyo pia amewataka wakazi ambao bado hawajapata vitambulisho vya kitaifa pamoja na kadi za usajili wa wapigakura kuhakikisha wanavipata mapema ili wawe tayari kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Cherargei amesema ushiriki wa wananchi katika uchaguzi unategemea maandalizi mapema, akiwahimiza wale ambao hawajakamilisha taratibu za usajili wa wapigakura kuchukua hatua kabla ya kipindi cha uchaguzi.
Cherargei amesisitiza kuwa kwa upande wao, wanaendelea kujenga mtandao wa kisiasa na kuwa na imani kwamba uungwaji mkono wao kwa Rais Ruto utamwezesha kupata muhula mwingine wa uongozi.

