Seneta wa Nandi, Samson Cherargei, amepinga vikali kile alichokiita mapendeleo katika uteuzi wa wagombea wa vyama vya kisiasa, akitaka mchakato huo kuangaziwa kwa makini
Cherargei amesema uteuzi wa wagombea unapaswa kuzingatia sifa, uwezo na uaminifu kwa chama, badala ya viongozi wa vyama kuwapendelea watu wa karibu, wakiwemo wapenzi au jamaa zao.
Amesema wanachama wanaohudumu na kukiunga mkono chama kwa muda mrefu wanapaswa kupewa nafasi ya kushindania tiketi za vyama kupitia mchakato wa haki na wazi. Ameonya kuwa matumizi mabaya ya michakato ya uteuzi yanaweza kuzua malalamiko na migawanyiko miongoni mwa wanachama wa vyama vya kisiasa.
APERIT FM,HII NI YETU

