You are currently viewing SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO

SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO

Naibu Gavana wa Pokot Mgharibi Robert Komole na viongozi wengine wa kaunti

Serikali ya Kaunti ya Pokot Magharibi imefanya mkutano na washikadau mbalimbali kuweka mikakati ya mapema ya kujitayarisha na kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa katika msimu wa Oktoba hadi Desemba 2026.

Mkutano huo uliwaleta pamoja maafisa wa kaunti kutoka idara mbalimbali, Mashirika mbalimbali, wataalamu wa hali ya hewa pamoja na washikadau wengine wa masuala ya maafa na mazingira.

Washikadau

Miongoni mwa mikakati inayozingatiwa ni kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema, kufanya tathmini ya maeneo yaliyo katika hatari, kuandaa mipango ya uokoaji na kuongeza uhamasishaji wa wananchi kuhusu hatua wanazopaswa kuchukua kabla na wakati wa mvua kubwa.

Vallary Cheyech, Meneja wa Aperit FM

Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi yafanya makutano na washikadau mbalimbali kuweka mikakati ya kujitayarisha na kukabiliana na mvua ya elnino.

Viongozi wa kaunti ya Pokot magharibi

APERIT FM, HII NI YETU