Serikali imetenga shilingi bilioni 2.1 kufanikisha mpango wa kuwalinda wafugaji dhidi ya hasara, kabla ya kuanza kwa mvua zinazotarajiwa za El Niño.
Kulingana na waziri wa kilimo Mutahi Kagwe mpango huo unalenga kupunguza athari za mvua hizo kwa sekta ya mifugo na kuhakikisha wafugaji wanaendelea kuwa na uwezo wa kuhifadhi mifugo yao na kujikimu wakati wa hali ngumu ya hewa.
Amesema hatua hiyo inatarajiwa kusaidia jamii za wafugaji kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mafuriko, uharibifu wa malisho na miundombinu, pamoja na hatari nyingine zinazohusiana na mvua nyingi. Amesema maandalizi ya mapema ni muhimu katika kulinda maisha, mifugo na maisha ya kiuchumi ya jamii zinazotegemea ufugaji.
APERIT FM,HII NI YETU

