Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa, Gladys Boss Shollei, amesema viongozi wanapaswa kushirikiana na washirika wenye mtazamo unaofanana na wao, na kuwa ndani ya serikali, ili waweze kutekeleza huduma na kuleta matokeo yanayowanufaisha Wakenya.
Shollei amesema ushirikiano wa kisiasa ni sehemu ya historia ndefu ya siasa za Kenya, akitaja miungano mbalimbali iliyowahi kuundwa nchini, ikiwemo Rainbow, NASA, CORD, Azimio na Kenya Kwanza.
Amesema serikali jumuishi ni mwendelezo wa utamaduni huo wa kuunda ushirikiano wa kisiasa, akisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuweka mbele maslahi ya Wakenya na kushirikiana katika kutekeleza ajenda za maendeleo.
Ametoa wito kwa viongozi kuacha misimamo inayoweza kuwagawa wananchi na badala yake kujenga ushirikiano utakaowezesha serikali kutoa huduma bora na kufikia malengo ya maendeleo.

