You are currently viewing WAKILI KOSGEI AWARAI WAKAAZI WA NANDI KUMPIGIA KURA

WAKILI KOSGEI AWARAI WAKAAZI WA NANDI KUMPIGIA KURA

Mwaniaji wa kiti cha ugavana wa Nandi, wakili Allan Kosgey, amewataka wakazi wa Nandi Hills kuunga mkono   azma yake ya kuwania uongozi wa kaunti hiyo.

Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Kosgey amesema anategemea kupata uungwaji mkono wa wenyeji wa nandi hills, huku akitoa muhtasari wa mpango wake wa maendeleo kwa eneo hilo na kaunti ya Nandi kwa ujumla.

Kosgey amesema uongozi wake utalenga kuharakisha maendeleo na kushughulikia changamoto zinazowakabili wakazi.

Aidha amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao kwa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kutekeleza ahadi zao.