You are currently viewing TSC YATAKIWA KUZINGATIA MAZINGIRA NA HAKI ZA WALIMU WAKATI WA UHAMISHO

TSC YATAKIWA KUZINGATIA MAZINGIRA NA HAKI ZA WALIMU WAKATI WA UHAMISHO

Mbunge wa Marakwet Magharibi, Timothy   Toroitich, ameitaka tume ya huduma za walimu (tsc) kuhakikisha kuwa uhamisho wa walimu nchini unazingatia masuala ya kibinadamu na mazingira halisi wanayopitia walimu pamoja na familia zao.

Toroitich amekosoa vikali uhamisho wa walimu unaofanywa bila kuzingatia hali zao binafsi, akisema maamuzi kama hayo yanaweza kuwa na athari kubwa kwa walimu, familia zao na hata utoaji wa elimu shuleni.

Amesema masuala muhimu kama vile hali ya afya ya mwalimu, mahitaji ya familia na mazingira mengine maalum yanayoweza kumfanya mwalimu ashindwe kuhamia kituo kingine yanapaswa kuzingatiwa kabla ya uhamisho kufanywa.
‎amesema walimu ni sehemu muhimu ya mfumo wa elimu na wanahitaji kutendewa kwa haki na utu,   akisisitiza kuwa uhamisho haupaswi kuwa chanzo cha kuvuruga maisha ya familia za walimu

 Amesema, badala ya kutumia mfumo wa jumla unaoweza kuwahusisha walimu wote kwa namna moja, mamlaka husika zinapaswa kuangalia mazingira ya kila mwalimu na kutoa nafasi kwa wale wenye changamoto maalum kueleza hali zao.