You are currently viewing TUNATAKA SERA SIO KAULI MBIU

TUNATAKA SERA SIO KAULI MBIU

Rais William Ruto amemjibu vikali aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua na viongozi wengine wa upinzani wanaoendeleza kauli mbiu ya One Term, akisema siasa za Kenya haziwezi kujengwa kwa kauli mbiu, porojo na maneno ya majukwani pekee.

Akizungumza katika kaunti ya embu rais Ruto amepuuza madai ya Gachagua kwamba atamfunza siasa, akisistiza kuwa yeye ni kiongozi aliye jijenga kisiasa kupitia juhudi zake mwenyewe na kwamba anaelewa vyema mahitaji ya wakenya.

Rais William Ruto amesema viongozi wanapaswa kuzingatia maendeleo na utekelezaji wa miradi ya kuwanufaisha wananchi badala ya kutumia muda mwingi katika siasa za mapema za uchaguzi.

Aidha amesisitiza uchaguzi mkuu ujao utategemea sera wala si kauli mbiu.