You are currently viewing UKAME YAATHIRI ENEO LA SIGOR

UKAME YAATHIRI ENEO LA SIGOR

Wakaazi wa Masol eneo bunge la Sigor katika kaunti ya Pokot Magharibi wamelalamikia kukithiri kwa hali ya ukame hali ambayo inafanya vigumu kuendeleza shughuli zao za kawaidia.

Wakiongozwa na chifu wa kata ya Masol Robert Lotumal, wakaazi hao wamesema kwamba hali hiyo imewapelekea kukadiria hasara baada ya kunyauka kwa mimea yao shambani na hata baadhi ya mifugo kufa wakitoa wito kwa serikali na wadau kuingilia kati kuhakikisha kwamba wanasaidika.

Lotumal amesema hali hiyo imepelekea kuathirika kwa shughuli za masomo kutokana na hali ya wakaazi wengi kuhama katika juhudi za kutafuta lishe ya mifugo wao na kufanya vigumu kwa wanao kuhudhuria vipindi vya masomo shuleni.