Wakazi wa vituo vya biashara vya Tapach na Sina sasa wanatarajiwa kunufaika na usalama ulioimarishwa baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa taa za barabarani.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo gavana Simon Kachapin amesema mradi huo, ambao ulikuwa sehemu ya ahadi ya kuboresha miundombinu katika maeneo ya biashara, unalenga kuongeza usalama, kuwezesha wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao hadi nyakati za usiku, pamoja na kuhakikisha mazingira salama kwa wafanyibiashara
Ameongeza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuimarisha miundombinu inayokidhi mahitaji ya wananchi, kukuza shughuli za kiuchumi na kuharakisha maendeleo endelevu katika maeneo mbalimbali ya kaunti.
Amewahimiza wananchi kutunza miundombinu hiyo ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa manufaa ya jamii kwa muda mrefu.

