Seneta wa Trans -Nzoia, Allan Chesang, amewataka viongozi wa kisiasa kuacha kuwatumia vijana kutekeleza vitendo vya vurugu na uhalifu wa kisiasa kwa manufaa yao.
Chesang amesema badala ya kuwahusisha vijana katika machafuko, viongozi wanapaswa kutumia rasilimali walizonazo kuwawezesha kupitia fursa za elimu, ajira, biashara na ujasiriamali ili kuboresha maisha yao.
Amesisitiza kuwa kuwawezesha vijana kiuchumi kutawapa matumaini ya maisha bora, kupunguza ushawishi wa kujiingiza katika vitendo vya kihalifu na kuchangia kudumisha amani, umoja na maendeleo ya nchi

