You are currently viewing WAFCON KUENDELEA LEO USIKU

WAFCON KUENDELEA LEO USIKU

Michuano ya kombe taifa bingwa Afrika kwa soka ya wanawake WAFCON inaendelea usiku wa leo, ambapo leo usiku, timu ya taifa ya kandanda Kenya Harambee Starlets, itashuka dimbani kukabana koo dhidi ya Algeria kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi A. Pambano hilo kati ya Kenya na Algeria, litang’oa nanga saa tano kamili usiku.

Ikumbukwe michuano ya WAFCON inachezewa nchini Morocco, na Harambee Starlets ilipoteza mechi za kwanza 2 dhidi ya wenyeji Morocco mabao manne kwa yai, na bao moja komboa ufe dhidi ya Senegal, na hivyo leo wanacheza tu kuheshimu kalenda ya FIFA.

Kwenye ratiba nyingine ya michuano ya WAFCON, leo saa tano kamili usiku, wenyeji Morocco watajaa uwanja kutoana kijasho na dhidi ya mabanati wa Senegal.