Waziri wa Utumishi wa Umma Geofrrey Ruku, amesema ama imani kuwa rais William Ruto atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 hata bila kupata uungwaji mkono kutoka eneo la Mlima Kenya Magharibi.
Akizungumza katika eneo la Kabartonjo Kaunti ya Baringo, Waziri Ruku amesema ushindi wa Rais William Ruto mwaka wa 2027, hautategemea kura za Mlima Kenya magharibi pekee.
Akitoa mfano uchaguzi mkuu wa mwaka 2013, ambapo rais mustaafu Uhuru Kenyatta, alimshinda hayati Raila Odinga licha ya tofauti ndogo ya kura.

