Uchaguzi mkuu ujao huenda ukakumbwa na machafuko iwapo wanasiasa wataendelea kuwatumia wahuni kuvuruga mikutano ya kisiasa na kuendeleza semi za chuki.
Kamishena wa iebc, alutalala mukhwana ameelezea hofu kwamba uchaguzi mkuu ujao uwenda usiakisi matakwa ya wakenya iwapo ghasia za kisiasa zitaendelea kulitikisa taifa.
Kamishna huyo, amekemea vitendo vya uhalifu na uhuni kuingilia mikutano ya kisiasa akisema kuwa wahuni wanafadhiliwa na wanasiasa.
Mukhwana aidha amesema kuwa wanasiasa watakaopatikana wakihusika na vitendo vya uhuni na matamshi mabaya watakabiliwa kisheria.

