Mwakilishi wa wadi ya Sitatunga, Simon Murei, amewataka wakazi wa Trans Nzoia kumuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kutafuta muhula wa pili wa uongozi.
Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Murei amesema wananchi wanapaswa kuendelea kuunga mkono serikali ya Rais Ruto ili kuipa nafasi ya kutekeleza ajenda zake za maendeleo.
Murei pia ametoa wito kwa jamii mbalimbali zinazoishi katika kaunti ya Trans Nzoia kudumisha amani na kuishi kwa ushirikiano, akisema umoja wa wananchi ni muhimu kwa maendeleo ya eneo hilo.
Amesisitiza umuhimu wa wananchi kuepuka migawanyiko ya kikabila na badala yake kushirikiana katika kujenga jamii yenye mshikamano.

