Mwaniaji wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Tranzoia Balozi Susan Nakhumicha ameendeleza harakati zake za kusaka uungaji mkono, akieleza sababu zinazomfanya aamini anafaa kuchaguliwa kama gavana wa kaunti hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2027.
Nakhumicha amewahimiza wakazi wa trans nzoia kuangazia rekodi yake ya utumishi, maono yake ya maendeleo na uwezo wa kuongoza kaunti hiyo.
Akizungumza na wakazi, Nakhumicha amesema analenga kuleta uongozi unaozingatia huduma bora, maendeleo na maslahi ya wananchi iwapo atapewa nafasi ya kuongoza Trans nzoia.
APERIT FM ,HII NI YETU

