Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, amewataka watalii na wawekezaji kusitisha safari na uwekezaji hapa nchini kwa madaia ya kuongezeka kwa visa vya utovu wa usalama hapa nchini.
Akizungumza mjini Kerugoya kaunti ya Kirinyaga, Gachagua amesema hali ya usalama nchini hairidhishi, akiwataka watalii Pamoja na wawekezaji kusubiri hadi mwaka ujao kabla ya kuzuru Kenya.
Kauli ya Gachagua inajiri siku chache tu baada ya chama chake cha DCP, kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou, Gachagua akisema ushindi huo, ni Ishara ya mwelekeo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027, amesema ushindani mkuu utakuwa kati yake Pamoja na rais William Ruto.

