You are currently viewing UHISPANIA NA URENO ZAWEKA MIADI KUKUTANA HATUA YA 16

UHISPANIA NA URENO ZAWEKA MIADI KUKUTANA HATUA YA 16

Bao la kichwa la mchezaji aliyetokea benchi Goncalo Ramos liliiwezesha Ureno kupenya katika hatua ya 16 bora ya kombe la dunia kwa ushindi wa 2 – 1 baada ya mpambano wa kusisimua dhidi ya Croatia.

Ramos aliunganisha pasi maridadi kutoka kwa Rafael leao katika dakika ya nne ya muda wa majeruhi na kuizima timu ya Croatia ambayo ilikuwa imetengeneza sehemu kubwa ya nafasi za kufunga mabao katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye joto kali la jioni jijini Toronto.

Croatia walidhani wamesawazisha katika sekunde za mwisho za mchezo lakini bao la Josko Gvardiol likafutwa kwa kuwa lilikuwa la kuotea. Wakroatia waliachwa wamidomo wazi kufuatia uamuzi huo, huku wachezaji wa Ureno wakisherehekea.

Mechi hiyo pia iliwakutanisha wachezaji wawili wenye uzoefu mkubwa na ambao wanacheza mashindano yao ya mwisho ya kimataifa, Cristiano Ronaldo wa Ureno mwenye umri wa miaka 41, ambaye hili ni kombe la lake la sita, na Luka Modric wa Croatia mwenye umri wa miaka 40 anayeshiriki kwa mara ya tano.