Mgombea wa kiti cha uwakilishi wa wanawake, Rebby Chepchumba Sebei, amesema afisi hiyo hupokea fedha za maendeleo zinazokadiriwa kuwa shilingi milioni 40 kwa mwaka, ambazo zinaweza kutumika kubadilisha maisha ya wanawake na jamii kwa jumla.
Sebei amesema fedha hizo zinapaswa kutumiwa kwa njia inayolenga mahitaji halisi ya wananchi, hususan kina mama ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Amesema iwapo rasilimali zinazotengewa ofisi hiyo zitatumiwa ipasavyo na kwa uwazi, zinaweza kusaidia wanawake kuanzisha na kukuza biashara ndogo ndogo, kupata mafunzo ya ujuzi pamoja na kuwawezesha kujitegemea kiuchumi.
Sebei amesisitiza umuhimu wa kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha wanawake wananufaika moja kwa moja na fedha za maendeleo, badala ya rasilimali hizo kupotea bila kuleta mabadiliko yanayoonekana katika jamii.
Amewataka wananchi kuchagua viongozi wenye uwezo wa kusimamia rasilimali za umma kwa uwajibikaji na kuhakikisha fedha zinazotengewa maendeleo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
APERIT FM,HII NI YETU

