Mbunge wa Soy, David Kiplagat, ameelezea wasiwasi kuhusu mfumo wa utoaji ajira katika ujenzi wa hospitali mpya ya Rufaa eneo la Kiplombe.
Kiplagat amesema wakazi wa eneo hilo wanapaswa kupewa kipaumbele katika fursa za ajira zinazotokana na mradi huo, akisisitiza kuwa maendeleo ya mradi huo yanapaswa pia kunufaisha jamii inayouzunguka.
Mbunge huyo amefichua kuwa tayari amemwandikia waziri wa afya Aden Duale , akiwasilisha malalamiko hayo na kutaka suala la ajira kwa wenyeji lishughulikiwe.
Kiplagat amesema atafuatilia suala hilo kwa karibu ili kuhakikisha wakazi wa soy na maeneo jirani wanapata nafasi ya kunufaika na fursa zinazotokana na ujenzi wa hospitali hiyo
APERIT FM,HII NI YETU

