Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia, George Natembeya, ameibua wasiwasi kuhusu madai ya usajili wa raia wa Uganda kama wapiga kura nchini Kenya, akisema hatua hiyo inaweza kutumiwa kuathiri matokeo ya uchaguzi katika kaunti za mpakani.
Natembeya amesema serikali na taasisi zinazohusika na uchaguzi hazipaswi kuruhusu raia wa kigeni kuingizwa katika sajili ya wapiga kura kwa lengo la kushawishi uchaguzi wa Kenya.
Akiangazia maeneo ya mpakani, ikiwemo Trans nzoia, gavana huyo amesisitiza kuwa ni lazima hatua zichukuliwe kuhakikisha sajili ya wapiga kura inakuwa na raia wanaostahili kisheria kupiga kura nchini.
Amesema suala hilo linapaswa kuchunguzwa kwa kina ili kulinda uadilifu wa uchaguzi na kuhakikisha kila kura inayopigwa ni ya mpiga kura anayestahili.
APERIT FM ,HII NI YETU

