You are currently viewing LONYANG’APUO ATOA WITO WA KUMUUNGA MKONO RAIS RUTO

LONYANG’APUO ATOA WITO WA KUMUUNGA MKONO RAIS RUTO

Mwenyekiti wa shirika la Riftvalley Water Works ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha ugavana  Profesa John Krop Lonyang’apuo, ,ametoa wito kwa wakazi wa Chepareria, na kaunti ya  Pokot Magharibi kwa ujumla , kumuunga mkono rais William   Ruto katika azma yake ya kuwania muhula wa pili kwenye uchaguzi ujao

Akizungumza katika eneo la Naramam, Lonyang’apuo pia amehimiza wafuasi wake kuunga mkono vuguvugu lake la kisiasa la 5g.

Profesa Lonyang’apuo amesema kaunti hiyo inaunga mkono kikamilifu azma ya rais ruto  huku akiwataka wakazi wa kaunti hiyo kudumisha mshikamano na kuunga mkono msimamo wao wa kisiasa kuelekea uchaguzi ujao.

APERIT FM,HII NI YETU