You are currently viewing USHIRIKIANO BAINA YA CHAMA CHA ODM NA UDA UTAENDELEA KUDUMU ASEMA  MBUNGE WA TURKANA KUSINI JOHN ARIKO

USHIRIKIANO BAINA YA CHAMA CHA ODM NA UDA UTAENDELEA KUDUMU ASEMA  MBUNGE WA TURKANA KUSINI JOHN ARIKO

Mbunge wa Turkana Kusini, Dkt. John Ariko Namoit, amesema Kaunti ya Turkana itaendelea kuwa ngome ya chama cha ODM na kwamba wananchi wa kaunti hiyo watachagua gavana kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

‎Dkt. Ariko amesema viongozi wa ODM kutoka Turkana wameamua kuendelea kushirikiana na serikali pana (Broad-Based Government), akieleza kuwa ushirikiano huo utaendelea kufuatia mwelekeo ulioanzishwa na aliyekuwa kiongozi wa chama hicho, Raila Odinga.

‎Aidha amesisitiza kuwa wataendelea kuiunga mkono serikali ya Rais William Samoei Ruto, akisema ushirikiano kati ya ODM na serikali umekuwa na manufaa kwa wananchi wa Turkana kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za umma.