Kufuatia hatua ya rais William Ruto, kuzindua rasmi mazungumzo ya kitaifa, kuhusu mpango wa maendeleo wa mwaka 2060, wandani wake kwenye kaunti ya Busia wamekuwa wa hivi punde kuipongeza hatua hiyo wakitaja kuwa bora katika ustawi wa nchi.
Kulingana na mwenyekiti wa chama UDA tawi la Busia, Maurice Chetambe, hatua hiyo ni hakikisho kuwa taifa liko katika nafasi bora kuimarika kiuchumi, sawa na mataifa mengine yaliyoimarika mfano Singapore. Kauli ambayo imetolewa pia na mwandani wa rais Ruto Isaac Alukwe.
Aidha wakizungumzia maswala mengine kwenye eneo bunge la Butula, viongozi hao aidha wamewashtumu wanachama wa ngazi za juu katika chama cha UDA kwenye kaunti hiyo ya Busia, kwa madai ya kusababisha mchanganyiko chamani, kwa kuidhinisha wagombea wa nyadhifa za kisiasa kwenye kaunti hiyo wasio kuwa wanachama.
Wiki iliyipotia naibu mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Kevin Lunani, katika mkutano wa hadhara na waziri mwenye maamlaka makuu Musalia Mudavadi, alimuidhinisha Gavana Paul Otwoma, kuwa mgombea ugavana kwenye kaunti hiyo ya Busia katika mpango wa serikali jumuishi.
Aidha Balozi Ababu Namwamba, alimuhidhinisha Otwoma siku mbili zilizopita katika mkutano wa UDA kule Budalangi kuwania nafasi hiyo.
APERIT FM, HII NI YETU

