You are currently viewing SANAMU YA UKUMBUSHO YAKE RAILA ODINGA.

SANAMU YA UKUMBUSHO YAKE RAILA ODINGA.

Serikali kupitia jeshi la ulinzi la Kenya KDF inatarajkiwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa Kaburi la kumbukumbu la aliyekuwa Waziri Mkuu hayati Raila Odinga, wenye thamani ya shilingi milioni 30, baada ya familia yake kukabidhi rasmi eneo litakalo jengwa.

Akizungumza katika hafla ya makabidhianio mwanawe Odinga, Raila Odinga Junior, amesema urithi mkubwa wa babake ulijikita katika Demokrasia, Amani na Katiba ya Kenya.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Septemba, kabla ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo chake Raila Odiga.

Alifariki dunia tarehe 15 Oktoba mwaka wa 2025 kutokana na mshtuko wa moyo.