Maandalizi ya sherehe za kitaifa za mashujaa katika kaunti ya Uasin Gishu yameingia hatua za mwisho, huku viongozi wa kaunti wakihakikisha utayari wa miundombinu na huduma muhimu
Naibu gavana wa uasin gishu, wa kaunti hiyo Evans Kapkea, amesema maandalizi yanaendelea kama yalivyokusudiwa na kwamba kaunti iko tayari kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali nchini watakaohudhuria sherehe hizo.
Kapkea amesema serikali ya kaunti inaendelea kushirikiana na serikali ya kitaifa pamoja na wadau wengine kuhakikisha maandalizi ya mashujaa day yanafanyika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika.
Wakati huo uo, amesema kaunti hiyo imeanza kuweka mkazo maandalizi ya uwezekano wa kuwa mwenyeji wa shughuli za soka za kiwango cha bara.
Kapkea amefichua kuwa maafisa kutoka shirikisho la soka Afrika, CAF, pamoja na maafisa wanaohusika na AFCON, tayari wametembelea kaunti hiyo kwa ajili ya kutathmini uwanja wa Kipchoge Keino na vituo vingine vya mazoezi.

