You are currently viewing MWAKILISHI WA AKINA MAMA KAUNTI YA TURKANA ATETEA AJENDA ZA SERIKALI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO

MWAKILISHI WA AKINA MAMA KAUNTI YA TURKANA ATETEA AJENDA ZA SERIKALI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO

Mwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Turkana, Cecilia Asinyen, ameshabikia mipango ya serikali katika kusawazisha miradi ya maendeleo kwenyesehemu tofauti ya nchi

Asinyen ametolea mfano kaunti ya Turkana ambayo kwa muda mrefu ilitengwa kimaendeleo kutokana na ukosefu wa nia njema miongoni mwa viongozi.

Amesema wanawake kutoka kaunti zote arobaini na saba nchini wataendelea kuzuru sehemu tofauti ya nchi kuuza sera za serikali na kushinikiza uungwaji mkono wa Rais William Ruto kuelekea uchaguzi ujao

Amewataka wafuasi wa mrengo wa kenya kwanza kuendelea kuwa watulivu na kujipanga kisiasa, akisema serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itaimarisha imani ya wananchi kwa uongozi wa Rais Ruto kabla ya uchaguzi wa 2027.

Wakati huo uo amewataka wakenya kujitnga na hulka ya kuchagua rais kutoka eneo moja akisema hulka hio imechangaia kuendelea kushamiri kwa ukoloni mambo leo huku wananchi wakikosa maendeleo stahiki