Wauguzi katika kaunti ya elgeyo marakwet wamejiunga na mgomo wa kitaifa wa wahudumu hao wa afya, wakilalamikia kile walichokitaja kuwa ni kutotekelezwa kwa makubaliano ya muda mrefu kuhusu maslahi na mazingira yao ya kazi.
Wauguzi hao wameilaumu baraza la magavana , kwa kuwa kikwazo kikuu katika juhudi za kumaliza mgogoro huo,kwa kudinda kuidhinisha makubaliano ya kurejea kazini, hatua ambayo imechelewesha kumalizika kwa mgomo unaoathiri utoaji wa huduma za afya katika kaunti mbalimbali.
Aidha, wauguzi hao wamedai kuwa baraza hilo limeshindwa kutekeleza makubaliano ya pamoja ya mishahara na masharti ya kazi cba ya mwaka 2017, ambayo yalilenga kuboresha mishahara, marupurupu na mazingira ya kazi kwa wauguzi nchini.
Wameitaka serikali za kaunti na wadau husika kushughulikia malalamiko yao kwa haraka ili kuwezesha kurejea kazini na kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma muhimu za afya

