You are currently viewing UHISPANIA YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA UBELGIJI

UHISPANIA YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA UBELGIJI

Uhispania imefuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji katika mechi ya robo fainali iliyochezwa mjini Los Angeles.

Magoli ya Uhispania yalifungwa na Fabian Ruiz dakika ya 30, na Mikel Merino katika dakika ya 88. Kwa upande wa Ubelgiji, Charles De Ketelaere aliipatia timu yake goli la kusawazishia katika dakika ya 41.

Kibarua kikali dhidi ya Ufaransa

Kwa ushindi huo, Uhispania sasa itakutana na Ufaransa katika hatua inayofuata ya Kombe la dunia 2026. Wakati huo huo, baadaye leo itachezwa mechi ya robo fainali ambapo Norway itapimana nguvu na England, huku macho mengi yakielekezwa kwenye washambuliaji Erling Haaland na Harry Kane.