Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong ametoa wito kwa magavana kutoka kaunti za bonde la Kerio kuhakikisha masoko yote yanafunguliwa ili kutoa fursa kwa wenyeji kuendeleza shughuli za kibiashara
Kulingana na Lochakapong asilimia kubwa ya wenyeji wanategemea mifugo kama kitega uchumi na ufunguzi wa masoko hayo utatoa fursa kwa jamii kujipatia kipato na kuendesha shughuli zao za kila siku

