You are currently viewing NORWAY NA UINGEREZA ZAFUZU KWA ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA

NORWAY NA UINGEREZA ZAFUZU KWA ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA

Norway imefuzu kwa robo fainali ya kombe la Dunia kwa kuishinda Brazil 2-1. Uingereza nayo imesonga mbele katika robo fainali kwa kuishinda wenyeji mwenza Mexico 3-2

Norway imefuzu kwa robo fainali ya kombe la Dunia kwa kuishinda Brazil 2-1. Erling Haaland alifunga mabao mawili ya dakika za mwisho na kuipeleka Norway katika robo fainali ya kwanza ya kombe la dunia. 

Matokeo hayo yamewafanya mabingwa mara tano Brazil kutolewa mapema zaidi tangu 1990.

Kipa wa Norway, Orlan Nyland, alionyesha mchezo wa kuvutia na kuokoa penalti katika kipindi cha kwanza kutoka kwa Bruno Guimaraes kabla ya Haaland kufunga mara mbili katika dakika 11 za mwisho na kuwashangaza Brazil katika uwanja wa metlife.

Neymar ambaye alirudisha bao moja katika dakika za mwisho kupitia penalti ya pili ya Brazil katika mechi hiyo, amedokeza anajiandaa kustaafu soka la kimataifa.

Mabao mawili ya Haaland yamemuwezesha kuifikia idadi ya mabao saba ya Lionel Messi katika mashindano hayo huku Norway ikijikatia tiketi ya kupambana na wenyeji wenza Mexico au Uingereza katika robo fainali huko Miami mnamo Julai 11.

Kwa Brazil, ambayo ilimwajiri Carlo Ancelotti katika jaribio la kufikisha ukame wa Kombe la Dunia wa miaka 24, ni mashindano ya sita mfululizo ambapo imetolewa na timu pinzani kutoka barani Ulaya.

Uingereza imesonga mbele katika robo fainali kwa kuishinda Mexico 3-2. Uingereza sasa itamenyana na Norway katika pambano litakalochezwa Jumamosi Julai 11 huko Miami.