You are currently viewing JIANDAENI KWA KIPINDI CHA BAA LA NJAA ASEMA ALIYEKUWA GAVANA WA POKOT MAGHARIBI JOHN LONYANGAPUO

JIANDAENI KWA KIPINDI CHA BAA LA NJAA ASEMA ALIYEKUWA GAVANA WA POKOT MAGHARIBI JOHN LONYANGAPUO

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya  Pokot Magharibi  Profesa John Krop Lonyang’apuo, amesema kuwa mabadiliko yanayoshuhudiwa katika eneo la north rift  ni ushahidi kwamba juhudi za serikali za kurejesha amani zimezaa matunda.

Amesema maeneo ambayo hapo awali yalikuwa yakikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wahalifu na wizi wa mifugo sasa yameanza kushuhudia utulivu, hali ambayo imewaruhusu wananchi kurejea katika shughuli zao za kilimo, ufugaji na biashara bila hofu.


‎Amesema ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa, viongozi wa eneo hilo na wananchi umechangia pakubwa katika kupunguza visa vya uhalifu na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Aidha ametoa wito wa kuanzishwa mikakati ya uzambazaji wa chakula kwenye maeneo yaliyoathiriwa na ukame