You are currently viewing UINGEREZA NA NORWAY ZAWANIA KUTINGA NUSU FAINALI

UINGEREZA NA NORWAY ZAWANIA KUTINGA NUSU FAINALI

Timu za Uingereza na Norway zitachuana baadaye leo katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia. Mechi hiyo itashuhudia mchuano mkali wa washambuliaji wawili nyota, Erling Haaland wa Norway na Harry Kane wa Uingerza.

Kocha wa Norway, Stale Solbakken, amesema Haaland ndiye mchezaji muhimu zaidi kwa timu yake, kama vile Kane alivyo muhimu kwa Uingereza.

Kiungo wa Uingereza Morgan Rogers amesema moja ya changamoto kubwa kwa timu yake itakuwa kumzuia Haaland, huku Nico O’Reilly, akisisitiza kuwa njia bora ya kumdhibiti ni kuzuia asipewe mpira katika maeneo hatari.

Mechi kali nusu fainali

Mshindi wa mchezo huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Hard Rock mjini Miami nchini Marekani, atafuzu kwenda hatua ya nusu fainali na atakutana na mshindi kati ya Argentina na Uswisi.