You are currently viewing GAVANA KACHAPIN ATAJWA KUWA MIONGONI MWA MAGAVANA BORA NCHINI KULINGANA NA UTAFITI WA INFOTRACK

GAVANA KACHAPIN ATAJWA KUWA MIONGONI MWA MAGAVANA BORA NCHINI KULINGANA NA UTAFITI WA INFOTRACK

Gavana wa Kaunti ya West Pokot, Simon Kachapin, ameorodheshwa katika nafasi ya sita miongoni mwa magavana 47 nchini kwa utendaji bora katika maendeleo, kulingana na matokeo ya utafiti wa hivi punde wa infotrak.

‎Kwa mujibu wa utafiti huo, West Pokot imepiga hatua katika sekta mbalimbali muhimu zikiwemo ujenzi wa miundombinu, huduma za afya, elimu, kilimo, uboreshaji wa barabara pamoja na utoaji wa huduma kwa wananchi.

‎Matokeo hayo yanatajwa kuwa ishara ya maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa katika kaunti hiyo, huku viongozi wa kaunti wakieleza kuwa wataendelea kushirikiana na wananchi ili kuimarisha zaidi maendeleo na kuboresha maisha ya wakazi wa West Pokot.

‎Anayeongoza orodha hiyo ni gavanaIrungu Kang’ata wa muranga,George Natembeya – Tranzoia,Kimani wa matangi – Kiambu,Gladys Wanga wa Homabay,Mutula Kilonzo Juniour – Makueni,weasly Rotich – Elgeiyo Marakwet,Anyang nyong’o wa Kisumu, Kisha Simon Kachapin wa West Pokot

‎Mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Gavana Kachapin kupitia ukurasa wake wa facebook amewashukuru wakazi wa kaunti hiyo kwa kuendelea kumuamini na kumpa ushirikiano katika uongozi wake.

‎Kachapin amesema kutambuliwa kama gavana wa sita bora nchini kati ya magavana 47 katika Tathmini ya Utendaji ya Infotrak countytrak 2026 ni ishara kwamba juhudi za maendeleo zinazotekelezwa katika kaunti hiyo zinazaa matunda.

‎Amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa wananchi, kujitolea kwa watumishi wa umma na wahudumu wa afya, mchango wa Bunge la Kaunti pamoja na washirika wa maendeleo