Gavana wa kaunti ya Egeyo Marakwet, Wisley Rotich,ameitolea mwito wizara ya usalama kuendeleza mchakato wa kuhakikisha silaha zote haramu zilizo mikononi mwa raia zinarejeshwa ili kushuhudiwa amani ya kudumu
Akizungumza katika eneo la Kamoi Marakwet Magharibi Gavana Rotich amesema utwaaji wa silaha hizo kutasaidia kuhakikisha maendeleo inafika mashinani kwa faida ya wananchi
Aidha ameonya kuhusu kauli za viongozi kwenye majukwaa tofauti ya kisiasa akisema huenda zikachangia kugawanya taifa kwa misingi mbalimbali
Amemsuta aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, kutokana na kauli zake za kuchochea umma kwa misingi ya kikabila,akisema viongozi wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika masuala ya maendeleo na changamoto zinazowakabili wananchi, badala ya kujihusisha na kauli zinazochochea mijadala ya kisiasa.
APERIT FM ,HII NI YETU

