Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, amesema vuguvugu la Linda Mwananchi litaendelea kuwa na umoja, licha ya uhasama wa kisiasa unaoikumba vuguvugu hilo.
Akizungumza mjini Homabay, Sifuna amesema kuwa kulikuwa na juhudi za kuvuruga mkutano wao, kwa kufungwa kwa baadhi ya barabara ya kuelekea homabay mjini.
Hata hivyo, amesema wakaazi walijitokeza kwa wingi na kufungua barabara hizo, na hivyo kuwezesha mkutano wao kuendelea.
Kwa mujibu wa Sifuna, vuguvugu hilo limefanya ziara katika maeneo mbalimbali nchini, kuanzia Pwani hadi Magharibi, uku akidai kuwa rais William Ruto, hana uungwaji mkono mkubwa katika baadhi ya maeneo waliyoyazuru.
Sifuna aidha amesema alianza kutofautiana na ODM, baadha ya kifo cha mwalimu na mwanablogu, Albert Ojwang, aliyefariki dunia mikononi mwa maafisa wa polisi.
Sifuna amedai kuwa baada ya kukamatwa na baadae kufariki dunia kwa Ojwang, kulikiuka makubaliano yaliyokuwapo kati ya chama hicho na serikali kuhusu kukomeshwa kwa mauaji zaidi nchini.
Haya yanajiri huku baadhi ya viongoz wa chama cha ODM kule Luo Nyanza, wamewashtumu viongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi, kwa madai ya kuchochea vurugu katika mikutano yake ya kisiasa wakidai kuwa hatua hiyo, ni sehemu ya mpango mpana ya kuharibu picha ya chama hicho.
Akizungumza mjini Kisumu gavana wa Homabay Gladys Wanga, amelituhumu vuguvugu hilo linaloongozwa na seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna, kwa kuchochea vurugu, akisema viongozi wa kisiasa wanapaswa kuubiri umoja, na kuhakikisha kenya inabaki kuwa na amani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Ni kauli iliyotiwa mkazo na Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi, ambaye amesema vurugu zilizoshuhudiwa katika siku za hivi karibuni, hasa katika mikutano ya upinzani katika eneo la Nyanza, zinaonekana kuwa za kimfumo na kwamba zinalenga kuwachochea wananchi kuzua rapsha.
APERIT FM, HI NI YETU

