Seneta wa Kaunti ya Baringo, Vincent Chemitei, ameahidi kushinikiza walimu wanaofanya kazi katika eneo la bunge la Eldama Ravine kujumuishwa katika orodha ya wale wanaonufaika na marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu
Akizungumza kwenye hafla moja Chemitei amesema si haki kwa walimu wa eneo hilo kukosa posho hiyo ilhali wenzao katika maeneo mengine ya kaunti ya Baringo wanaendelea kunufaika
Amesisitiza kuwa mazingira ya kazi katika eneo hilo linapaswa kutathminiwa upya ili kuhakikisha walimu wanatendewa kwa usawa.
Seneta huyo amesema atawasilisha hoja hiyo kwa mamlaka husika, akisisitiza kuwa utoaji wa marupurupu ya mazingira magumu utasaidia kuwahamasisha walimu, kuboresha ustawi wao na kuinua kiwango cha elimu katika eneo la eldama ravine.

