Hotuba maalum kwa taifa iliyotolewa na Rais William Ruto , imeendelea kuibua hisia mbalimbali kutoka viongozi na wananchi, wengine wakiipongeza wengine wakiikosoa uku wengine wakikosa hasa kuelewa kilicho zungumziwa.
Lengo kuu la hutoba ya Rais William Ruto, lilikuwa kuliweka kenya katika mpango mpya wa ukuaji wa muda mrefu wa kiuchumi, uku mpango wa maendeleo ya vision 2030, ukikaribia kufikia kikomo.
Viongozi wakuu wa upinzani wakiongozwa na seneta wa kaunti ya nairobi edwin sifuna, wamekosoa vikali hotuba hiyo iliyochukua muda wa dakika 40, na kusisitiza kuwa ilipaswa kuangazia changamoto zinazo wakabili wakenya hivi sasa, badala ya kuelezea mipango ya siku zijazo.
Aidha kupitia taarifa yake sifuna amesema kuwa maendeleo ya nchi, hayawezi kutenganishwa na misingi ya katiba ya mwaka wa 2010.
Amesisitiza kuwa kabla ya kuzungumzia maendeleo ya kiuchumi, ni lazima taifa lizingatie maadili ya kidemokrasia, haki za kibinadamu, usawa, utawala wa sheria na haki ya kijamii kama yalivyo hainishwa kwenye katiba.

