You are currently viewing KAMAR ASHINIKIZA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA UCHIMBAJI MADINI

KAMAR ASHINIKIZA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA UCHIMBAJI MADINI

Seneta mteule, Profesa Margaret. Kamar, ametaka kufanyika mabadiliko ya sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya madini nchini ili kuwalinda wachimbaji wadogo wa madini na kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa kufuata sheria.

Kamar amesema wachimbaji wadogo wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa maeneo mbalimbali, lakini mara nyingi hukabiliwa na changamoto za ukosefu wa ulinzi wa kisheria, mazingira duni ya kazi na hatari zinazoweza kuepukika

 Ameeleza kuwa kuna haja ya kuweka mfumo utakaowapa leseni, mafunzo na ulinzi unaostahili ili waweze kufanya shughuli zao kwa usalama na tija,  akisisitiza umuhimu wa kudhibiti shughuli za uchimbaji wa madini kandokando ya mito, akionya kuwa uchimbaji usiodhibitiwa unasababisha uharibifu wa mazingira, kuongezeka kwa mmomonyoko wa ardhi na kuhatarisha vyanzo vya maji vinavyotegemewa na wananchi.