You are currently viewing VIONGOZI WA UPINZANI WAKOSOLEWA KWA KUPINGA MIPANGO YA SERIKALI BAADA YA RUWAZA YA MWAKA WA 2030

VIONGOZI WA UPINZANI WAKOSOLEWA KWA KUPINGA MIPANGO YA SERIKALI BAADA YA RUWAZA YA MWAKA WA 2030

Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, amewakosoa viongozi wa upinzani kwa kile amekitaja kuwa ukosefu wa ajenda na dira ya kuongoza maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika hafla moja, Murkomen amewataka wakenya kuunga mkono ajenda mpya ya kiuchumi ya rais william  ruto inayojulikana kama Beyond Vision 2030, akisema inalenga kuimarisha ukuaji wa uchumi, kuongeza fursa za ajira na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini.

Amesema serikali itaendelea kutekeleza sera na mipango inayolenga kuboresha maisha ya wananchi, huku akisisitiza kuwa maendeleo ya taifa yanahitaji umoja na uungwaji mkono wa wananchi kwa programu za maendeleo zinazotekelezwa na serikali.