You are currently viewing KAMATI YA MPITO, KUANDA MFUMO HURU WA WASIMAMIZI WA LIGI KUU NCHINI KENYA

KAMATI YA MPITO, KUANDA MFUMO HURU WA WASIMAMIZI WA LIGI KUU NCHINI KENYA

Shirikisho la soka hapa nchini la vilabu ambazo zinashiriki ligi kuu ya humu nchini, zimekubaliana kutengeneza kamati ya mpito ya wanachama 7 itakayoandaa mpango wa kuanzisha mfumo huru wa wasimamizi wa ligi kuu ya humu nchini katika msimu wa 2026-2027.

Kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti wa klabu ya Gor’ Mahia Ambrose Rachier, na itaanza kazi wiki ijayo.

Kamati hiyo itaanda mapendekezo ya kisheria na kiutawala, itakayowezesha ligi iyo kujisimamia bila kuathiri kuanza kwa musimu mpya, uliopangwa kuanzia Agosti tarehe 22 mwaka huu.

Aidha, rais wa shirikisho la soka humu nchini Hussein Mohammed, amesema kwamba mabadiliko hayo yatafanyika kwa ushirikiano na washika dau wote wa soka wakiwamo wadhami ni wa ligi.

Wakati huo huo ni kwamba viongozi wa vilabu ambavyo vinashiriki ligi hiyo wameeleza kuwa mageuzi yanaitaji kufuata taratibu za kisheria na kusisitiza kuwa hakuna mpango wa kusitisha msimu wa 2026-2027