Serikali imeonya wakenya kuhusu uwezekano wa mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya Elnino, ikisema hali hiyo inaweza kuhatarisha usalama wa wananchi na kusababisha uharibifu wa mali.
Akizungumza baada ya kuongoza kikao cha idara tofauti Naibu Rais amewataka wakenya kuwa waangalifu na kufuata maagizo na tahadhari zinazotolewa na idara na mashirika ya serikali, hasa katika maeneo yaliyo katika hatari ya mafuriko, maporomoko ya ardhi na athari zingine za mvua kubwa.
Ameweka wazi kwamba serikali inaangazia mikakati tofauti ikiwamo kuimarisha mifumo ya kupitisha maji taka na kuwahamasisha wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na idara ya utabiri wa hali ya anga
APERIT FM,HII NI YETU

