Chama cha kutetea maslahi ya walimu, knut, tawi la Pokot Magharibi, kimepinga madai ya walimu waliotumwa kufundisha katika shule za Junior Secondary JSS, kuhamishwa kutoka knut hadi Kuppet bila ridhaa yao.
Viongozi wa muungano huo, wakiongozwa na katibu wa Knut Dorcas Lotome, wamesema baadhi ya walimu waliokuwa wanachama wa knut wamejikuta wakihusishwa na Kuppet baada ya kutumwa kufundisha katika shule za JSS.
Walimu hao wanahoji utaratibu unaotumika, wakisisitiza kuwa haki yao ya kuchagua chama cha kuwakilisha maslahi yao inapaswa kuheshimiwa.
Viongozi hao pia wameilaumu tume ya kuajiri walimu, TSC, kwa kile wanachodai kuwa ni kuhusishwa na taratibu hizo za uhamisho wa walimu kutoka chama kimoja hadi kingine, bila kufuata taratibu zinazohitajika kisheria.
Wamesema iwapo suala hilo halitashughulikiwa kwa haraka, watalazimika kuandaa maandamano kupinga mchakato huo.
APERIT FM,HII NI YETU

