Mbunge wa sigor, peter lochakapong’, ametunukiwa rasmi heshima ya Chief Of The Order Of The Burning Spear (CBS), mojawapo ya tuzo za juu za kitaifa za heshima nchini
Lochakapong’ ametuzwa medali na cheti katika hafla rasmi iliyothibitisha uteuzi wake kuwa miongoni mwa waliotunukiwa heshima hiyo ya kitaifa.
Viongozi wengine waliotunukiwa heshima ya CBS ni seneta wa Pokot Magharibi, Julius Murgor; Mbunge wa Kapenguria, Samuel Moroto; seneta wa Turkana, James Lomenen; na seneta wa Elgeyo-Marakwet, William Kisang miongoni mwa viongozi wengi nchini
Heshima ya CBS ni sehemu ya mfumo wa kitaifa wa kutambua mchango, utumishi na huduma ya watu kwa taifa.
APERIT FM,HII NI YETU

