Gavana wa kaunti ya pokot magharibi Simon Kachapin ameongoza hafla rasmi ya kuwaapisha na kuwazindua wanachama wa bodi za hospitali za kaunti katika makazi rasmi ya Gavana Mjini Kapenguria.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Gavana Kachapin ameeleza kuwa bodi hizo zina jukumu muhimu la kuimarisha uongozi, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora za afya katika hospitali za kaunti, akiwataka wanachama hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwazi na kujitolea, huku wakitanguliza maslahi ya wananchi.
Amesisitiza kuwa serikali ya kaunti itaendelea kuwekeza katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu, kuimarisha huduma za matibabu na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya zilizo bora na zinazopatikana kwa urahisi.

