Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, amesema serikali ya Rais William Ruto inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kaunti ya trans Nzoia kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha ukuaji wa uchumi.
Akizungumza kwenye ziara ya maendeleo katika kaunti hiyo, Murkomen amesema serikali imewekeza katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara, upanuzi wa huduma za afya, uboreshaji wa sekta ya elimu pamoja na miradi ya maji na umeme inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
Ameeleza kuwa serikali pia inaendelea kuunga mkono sekta ya kilimo kupitia usambazaji wa mbolea ya ruzuku na programu nyingine zinazolenga kuongeza tija kwa wakulima na kuinua kipato cha wakulima katika eneo hilo.

