You are currently viewing LORI LA MCHANGA LAGONGA HOSIPITALI

LORI LA MCHANGA LAGONGA HOSIPITALI

Hali ya taaruki imetanda katika eneo la Kamorow, wadi ya Mnagei eneo bunge la Kapenguria katika kaunti ya Pokot Magharibi, barabara kuu ya Kitale-Kapenguria-Lodwar, hii ni baada ya lori moja la kiserikali ambalo limebeba mchanga kutoka kaunti ya Pokot Magharibi kuelekea Kaunti ya Trans-Nzoia, kupoteza mwelekeo na kusababisha ajali mbaya, ambayo imepelekea uharibifu wa mali ya thamani.

Akizungumza baada ya ajali hiyo dereva wa lori hilo ambaye hajapata jeraha lolote, anasema gari hilo lilipoteza mwelekeo baada ya kufeli breki, kisha kuligonga hosipitali la kibinafsi la Kape Pearl.

Hakuna majeruhi yoyote kwenye mkasa huo, kwani hosipitali hiyo haijaanza kufanya kazi rasmi ajali hiyo ikitokea, ila dereva huyo amekimbizwa katika hosipitalini ya Rufaa ya Kapenguria kwa huduma za kwanza na kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Maafisa wa trafiki wamefika kwenye eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi ili kubainisha chanzo cha ajali hiyo.

                                                                                              APERIT FM HII NI YETU