You are currently viewing KFS YAZINGATIA MATAKWA YAWENYEJI WA KAPTAGAT

KFS YAZINGATIA MATAKWA YAWENYEJI WA KAPTAGAT

Maafisa wa huduma ya misitu nchini KFS wamesogeza uzio wa msitu wa Kaptagat  umbali wa mita kadhaa baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu sehemu ya uzio iliyozuia barabara ambayo imekuwa ikitumiwa na wakazi kwa muda mrefu.

Hatua hiyo inafuatia kilio cha wakazi waliotaka barabara hiyo ya kihistoria ibaki wazi ili kuendelea kurahisisha usafiri na shughuli zao za kila siku.

‎Ujenzi wa uzio huo ni sehemu ya mpango wa kuhifadhi msitu wa kaptagat  , ambao pia unalenga kulinda msitu na kuhakikisha haki za matumizi ya jamii zinazingatiwa